Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumatatu, Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika: "Machi 16 ni kumbukumbu ya mwaka wa 33 wa mauji ya watu wa Halabja kwa silaha za sumu."
Ameongeza kuwa, "Baadhi katika nchi za Magharibi, ambao walimpa Saddam silaha angamizi za sumu, hawajajali kukumbuka tukio hilo."
Aidha Zarif ameongeza kuwa: "Zaidi ya raia 5,000 wasio na hatia waliuawa kwa gesi ya sumu." Amesema ni aibu kuwa nchi za Magharibi ambazo zilimpa Saddam silaha hizo za sumu sasa zinathubutu kudai kuwa eti Iran inavuruga uthabiti katika eneo, ili kufunika jinai zao.
Ikumbukwe kuwa, miaka 33 iliyopita mwezi huu wa Machi, utawala wa zamani wa Baath huko Iraq uliushambulia mji wa Wakurdi wa Halabja huko kaskazini mashariki mwa Iraq. Makumi ya ndege za kivita za utawala wa Saddam Hussein zilifanya mashambulizi ya kinyama kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wa Kikurdi wa mji wa Halabja.
342/